BOSS WA KAMPUNI YA APPLE AJIVUNIA KUWA SHOGA

Boss wa kampuni kubwa duniani ya Apple, leo ametangaza rasmi kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja.
Tim Cook amesema baada ya kimya cha muda mrefu ambacho amekuwa akitunzia siri hiyo, ameona namna alivyonufaika kutokana na kitendo cha watu wengine kujitoa sadaka kwa kijitangaza na kusisitiza kuwa anajivunia kuwa shoga na anajiona mwenye zawadi kubwa kutoka kwa Mungu.
Amesema kitendo cha yeye kama mkurugenzi wa kampuni hiyo kujitangaza kitawafanya wengine wenye hali kama yake wajione wako sawa na watu wengine.

Cook amesema marafiki zake wanajua kuhusu suala la yeye kuwa shoga, na haifanyi wamchukulie tofauti na watu wengine.
Kabla ya kujitangaza kumekuwa na fununu kuhusiana na Cook kuwa shoga, anakuwa mkurugenzi wa kwanza wa kampuni kubwa kujitangaza kuwa shoga ambapo mwaka jana alikuwa moja ya watu waliokuwa wanaunga mkono sheria ya kuwalinda wafanyakazi wasinyanyapaliwe kutokana na jinsia zao.
Cook amesema kwa kipindi kirefu watu wamekuwa wakificha juu ya jambo hilo maeneo ya kazi kuepuka unyanyapaa.
    Blogger Comment
    Facebook Comment