Uwepo wa daraja hilo unaweza kuwa ni neema kwa Watanzania wote na hata nchi za jirani kwani itarahisisha shughuli za kiuchumi na kibiashara kwa asilimia kubwa kwa kupunguza kero ya usafiri kwa wananchi.
Gazeti la HabariLEO liliripoti kuwa kwa sasa Shirika hilo lipo katika mazungumzo na wataalamu mbalimbali ili kuangalia uwezekano wa kujenga daraja hilo katika bandari ya Dar kwa upande wa Bara na Unguja kwa upande wa Visiwani
.
Mkurugenzi mkuu wa NSSF Ramadhan Dau alisema ujenzi wa daraja hilo si ndoto bali ni ukweli na tayari wameanza mazungumzo ya awali ili kutimiza malengo yao.
Umbali kati ya Dar na Zanzibar ni kilimeta73.43 sawa na maili45.62 hivyo kuwepo na mradi huo ni jambo linalowezekana kwani kuna madaraja marefu zaidi duniani yanayounganisha upande mmoja wa bahari na mwingine.
Kwa sasa daraja refu zaidi duniani kote ni lile la Danyang-Kushan lililopo nchini China ambalo lina umbali wa kilometa 165 sawa na maili102.4 ambalo lilifunguliwa Juni mwaka2011.
Blogger Comment
Facebook Comment