Ukuaji wa teknolojia unazalisha stori mpya kila siku ila leo huenda ukashtuka; unajua simu yako inaweza kukwambia siku yako ya kufa?
‘Macabre iPhone App’ ni application
ambayo unaweza kuiweka kwenye simu yako na jukumu ambalo utakuwa nalo ni
kuweka ratiba zako zote za siku nzima, application hiyo inapiga hesabu
halafu inakupa majibu siku zako ngapi zimesalia kuishi duniani.
Kali zaidi ni kwamba majibu utakayopewa
ya idadi ya miaka, miezi, wiki, siku na saa itakuwa inaonekana kwenye
screen lock, kwa hiyo kila unapotoa lock ya kwenye screen itakuwa
inaonekana hapo juu.
Majukumu yako ya siku ndiyo yataakayoamua siku ngapi utaishi.
Application hiyo inapatikana kwa simu za Apple zinazotumia iOS na Windows 8.
Unadhani uko tayari kuitumia application hii?
NIFUATE FACEBOOK
Blogger Comment
Facebook Comment