Beki wa kimataifa wa Argentina Marcos Rojo ambaye anaitumikia klabu
ya Manchester United atakaa nje ya uwanja kwa muda usiopungua wiki 12
ambazo ni sawa na miezi mitatu .
Taarifa hii mbaya inakuja baada ya beki huyo kuumia wakati wa mchezo
dhidi ya Manchester City uliopigwa jumapili kwenye uwanja wa Etihad
ambako United ililala 1-0 .
Taarifa hii kwa vyovyote itakuwa mwiba mchungu kwa mashabiki wengi wa
United ambao hadi sasa wanafahamu fika kuwa timu yao ni mojawapo kati
ya timu mbili ambazo zinaongoza kwa orodha ndefu ya wachezaji wenye
majeraha yanayowaweka nje ya uwanja .
Hali hii inafanya uchaguzi wa mabeki watakaokuwemo kwneye kikosi cha
United kuelekea kwneye mchezo wao dhidi ya Crystal Palce jumamosi ijayo
kuwa mgumu hasa ujkizingatia kuwa tayari timu hiyo inamkosa Chris
Smalling ambaye atakuwa nje kama adhabu ya ziada baada ya kuonyeshwa
kadi nyekundu , Phil Jones ambaye haijafahamika jeraha la ugoko
alilopata litapona lini huku Jonny Evans akiwa karibu kupona lakini
hawezi kuwahi mchezo wa jumamosi kwani anahitaji kuwa na utimamu wa
mwili thabiti kumfanya aweze kuwa kwneye hali ya kucheza mechi kwa
dakika 90 .
Blogger Comment
Facebook Comment