Yajue mapya kutoka kwenye klabu ya arsenal





THE+SQUADKlabu ya jijini London ya Arsenal itatangaza kumsajili kiungo wa Real Madrid Sami Khedira baada ya kufikia makubaliano na wawakilishi wa mchezaji huyo pamoja na viongozi wa Real Madrid .
Khedira kwa muda mrefu amekuwa hana nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Real Madrid hasa baada ya kusajiliwa kwa kiungo Toni Kroos na klabu ya Arsenal imekuwa ikisaka saini ya kiungo huyu ili kuboresha idara yake ya kiungo.
Kwa mujibu wa taarifa toka Hispania na England Arsenal imekubali kulipa paundi milioni 11 kwa ajili ya kiungu huyu mwenye asili ya Tunisia ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha cha Ujerumani kilichotwaa ubingwa wa dunia nchini Brazil mwaka jana .
Kiungo Mjerumani Sami Khedira atajiunga na Arsenal akitokea Real Madrid kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 11.
Kiungo Mjerumani Sami Khedira atajiunga na Arsenal akitokea Real Madrid kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 11.
Khedira angeweza kuondoka tangu wakati wa usajili wa majira ya joto lakini Arsenal na Madrid zilishindwa kufikia makubaliano juu yake na moja kati ya nafasi ambazo zimekuwa zikmtatiza kocha Mfaransa ni nafasi ya kiungo ambayo Khedira endapo akiwa fiti atakuwa na uwezo wa kuiboresha .
Tags :
    Blogger Comment
    Facebook Comment