Hii ilisikika kwenye AMPLIFAYA jana February 12, kijana mmoja Said maeneo ya Yombo amefariki, kisa kilianza alipoingia kwenye mkumbo wa vurugu, watu wakawaita Panya Rod, akapigwa na kuuawa.
Shuhuda mmoja alisimulia tukio lote lilivyokuwa; “Ninavyosikia
mwisho wa lami kulikuwa na shughuli, wakawa wameenda hapo. Kuna kundi
la vijana kutoka Sigara au Buza wakawa wamekuja katika shughuli, mmoja
alikuwa na panga akampiga Said ambaye ni marehemu, akamnyang’anya simu
yake.. wakawa wamefanya fujo pale…”
Wale vijana wa huku Machimbo wakawa wamerudi, kukatokea shughuli nyingine, kijana mwingine akawa amechanjwa viwembe na wale wa kundi la kule. Hawa wa huku wakasema mbona wanatuonea sana, kila tukienda wanatufanyia fujo? Inabidi na sisi tukawafanyie fujo..“
Wale vijana wa huku Machimbo wakawa wamerudi, kukatokea shughuli nyingine, kijana mwingine akawa amechanjwa viwembe na wale wa kundi la kule. Hawa wa huku wakasema mbona wanatuonea sana, kila tukienda wanatufanyia fujo? Inabidi na sisi tukawafanyie fujo..“
Kesho yake Said
hakwenda kazini akasema anaumwa, akaaga kuwa anaenda kununua dawa..
wakakutana na wenzie wakawafuata kule wakawafanyia fujo wakawapiga..
wakapiga simu Polisi, wengine wakapiga kelele ‘Jamani Panya Road’..
wanakijiji wakatoka, mwenye fimbo.. rungu.. wakawa wanawakimbiza wale wa
Machimbo. Said hakukimbia akasema mimi sijaiba ila nimeibiwa.. Mmoja
akarusha panga likampata Said akawa amedondoka chini wanakijiji
wakamvamia wakampiga“
Polisi
wakamchukua wakamuweka ndani ya gari Said akawa amezimia, baadaye Said
kuzinduka akamuona mvulana anayefahamiana naye akamwambia naomba
kawaambie nyumbani mimi naondoka nimekamatwa.. wakati anaongea wakampiga
rungu la kichwa akawa amekata kauli, hakuongea tena.. ni vilio tu
vilitawala pale mtaani“
Shuhuda huyo alimzungumzia Said kuwa ni kijana ambaye hakuwa na tabia yoyote ya wizi; “Ni kijana mdogo sana, hana tabia yoyote ile mbaya Said.. msiba umewauma wengi sana..“
Blogger Comment
Facebook Comment