Recent

JE! ULIPITWA NA MECHI ZA BPL USIKU WA JUMANNE YA FEBRUARY 10? NIMEKUWEKEA HAPA.






Mechi ya mojawapo ilikuwa ni kati ya Arsenal vs Liecister City, na mechi hiyo ilimalizika kwa matokeo ya 2-1 Arsenal ikiibuka kifua mbele baada ya wachezaji wake mahiri kuipatia timu yao ushindi huo katika uwanja wa nyumbani wa Fly Emirates.

Mabao hayo muhimu yalifungwa na Laurent Koscielny akipachika bao la kwanza kotokana na mpira wa kona.



Bao la pili lilipachikwa nyavuni na mchezaji Theo Walcott waada ya shuti zito lililo pigwa na Mesut Ozil na Kumshinda  mlinda mlango wa Liecister City na kuupangua kwa mikono miwili na kumkuta miguuni Theo Walcot na kutupia kimiani kwa shuti zito.
Goli la Liecister City lilifungwa mchezaji Kramaric mnamo dakika ya 61 na mechi kuweza kumalizika kwa matokeo hayo. TAZAMA HAPA


Mechi nyingine ilikuwa ni kati ya Liverpool vs Tottenham na matokeo yalimalizika 3 -2 Liverpool akiibuka kidedea.
Mabao yalifungwa na L.Markovic akipachika bao la kwanza mnamo dakika ya 15 kabla ya mshambuliaji mahiri ya Tottenham Hotspurs Harry Kane kuchomoa bao mnamo dakika ya 26, kipindi cha kwanza kilimalizika kwa matokeo hayo na baada tu ya n'gwe ya pili kuanza mnamo dakika ya 53 Captain wa Liverpool Steven Gerald kuipachikia timu yake bao la pili kupitia mkwaju wa penalt.
Hiyo pia ni kabla ya kiungo mahiri wa Tottenham Hotspurs Mousa Dembele kuipatia timu yake bao la pili nahivyo kupelekea mpaka dakika ya 82 matokeo kuwa ni 2-2.
Dakika ya 83 Striker mtukutu Super Mario Baloteli akaipatia timu yake bao la 3 na kuweza kuwalaza Tottenham Hotspurs na viatu kwa matokeo hayo ya 3-2.
TAZAMA HAPA


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment