Miongoni mwa stori zilizochukua headline
mitandaoni hata kwenye magazeti ni kuhusu picha ya hitmaker wa
‘Ndangushima’ Ommy Dimpoz akiwa na ex wa Diamond Platnumz ,Wema Sepetu
kitandani wamelala pamoja na picha zingine zilizozua mjadala mkubwa.
Sasa leo Feb 12 Ommy Dimpoz ame amplify kwenye Amplifaya ya Clouds FM na kusema ; ‘Ni
picha tu mimi naona kama ni picha zingine tu za kawaida, sasa
nimeshindwa kuelewa kwanini labda zimetengeneza sana stori kwasababu
mimi naona sio mara yangu kwanza kupiga picha na Wema hata uki google
utaona tunapicha nyingi sana kwa hiyo sijaelewa kwanini zimeleta stori
May be
nafikikiri zilizotengeneza stori zaidi ni hizi ambazo zinaonesha tuko
chumbani kwasababu mimi nilikuwa nimelala kiukweli na tulikuwa tunakaa
kwenye apartment moja nilikua nimeshtukia picha zipo kwenye mitandao
unajua unavyokaa kwenye apartment kwasababu tulienda kwenye matembezi
binafsi na washikaji wengine tulikua wengi wengi kidogo tulienda South
Africa unajua mnavyokaa kama familia kunakuwa na mambo ya utani utani
nimeshtukia tu picha zimeenea kwahiyo hata watu wakiniuliza ninawambia
wamuuliza aliyepiga picha hizo
Millardayo ; “…Wengi
wanafahamu kuwa wewe ni mshikaji wa Diamond Platnumz imekuaje sasa hivi
kuonekana kwenye picha na Ex wa Diamond Platnumz,Wema Sepetu…?”
Ommy Dimpoz ; “…Sidhani
kama kuna tatizo kwasababu hawa wote ni watu wangu nimefahamia nao siku
nyingi nimekuwa nao karibu katika kipindi tofauti kabla hawajakuwa
kwenye uhusiano mimi tayari ni watu wangu sidhani mimi nianze kuelezea
sijui ooh nilikuwa labda na Wema sehemu, Wema ni mshikaji wangu tangia
siku nyingi kwa hiyo hata kama alikuwa katika uhusiano na Diamond
yakatokea mahusiano yao pengine hayapo sasa hivi hayawezi kunifanya
mimi kuharibu ushikaji wangu kwasababu hivyo ni vitu vyao personal…“Alisema.
Blogger Comment
Facebook Comment