DULAYO APIGANA! MSIKILIZE KWENE U-HEARD YA LEO MARCH 19

Watu waamefikishiana taarifa kwamba msanii Dullayo ameonekana akipigana nje ya benki moja akiwa Mbeya huku akitokwa na damu pamoja na kuonekana ana majeraha, kuna ukweli kwenye hili?

Ishu ikafika mezani kwa Soudy Brown, kamtafuta Dullayo ili kujua ukweli wa ishu hii.. Dullayo amesema alikuwa Mbeya akaenda kuwasalimia rafiki zake eneo moja karibu na benki, wakati anapaki gari ghafla akavamiwa na jamaa aliekuwa anaendesha bodaboda na kuanza kumpiga.
Jamaa huyo alimjeruhi Dullayo, akaamua kutoa taarifa Polisi na pia kwenda Hospitali kupatiwa matibabu.
Ili kusikiliza bonyeza play hapa chini mtu wangu…

    Blogger Comment
    Facebook Comment