Recent

Rais wa Senegal Aomba jupunguza muhula wake!

Rais wa Senegal Macky Sall amependekeza kura ya maamuzi kuhusu kupunguzwa kwa muhula wake kwa miaka miwili,hatua ambayo ni kinyume na ile ya viongozi wengi wa Afrika ambao wanataka kusalia madarakani maisha.

Kulingana na gazeti la the Guardian nchini Uingereza,hatua hiyo inajiri wakati ambapo mataifa ya Benin,Rwanda,Burundi na Congo Brazzaville yanataka kubadilisha sheria ili viongozi wake waendelea kuhudumu kwa muhula wa tatu.
''Nilichaguliwa kwa miaka saba,lakini mwaka ujao nitapendekeza kufanyika kwa kura ya maamuzi ili kupunguza muhula wangu'',aliuambia mkutano na vyombo vya habari mjini Dakar.
Msimamo huo utasababisha kuangaziwa kwa katiba hususan kuhusu mamlaka na baadaye kuhusu vipengee vyengine vya kuimarisha demokrasia,alisema akiongozea kwamba angependelea kura hiyo kufanyika mwezi Mei mwaka ujao.
''Je,ushawahi kuona rais akipunguza muhula wake wa kutawala?'',basi mimi nitafanya ,Sall aliuambia mkutano huo akitoa ahadi hiyo ambayo ni baadhi ya ahadi zake alizotoa wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2012.

 Like PAGE yangu ya facebook ili usipitwe na lolote kutoka kwangu
Bofya hapa =>>>BOMGO PLANET
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment