Ujumbe huo unasema:
Naomba ieleweke kwamba, wasanii wa Tanzania tunatumia nguvu nyingi sana, ili kuweza kumudu sana hii.
Tunapambana sana, ili tujiweke katika mazingira ya kuonekana kama wasanii wa kisasa. Jitihada zetu zote zinategemea support ya Mashabiki wetu wanaotupenda. Wao wakipenda kazi zetu na kuzisupport, na sisi ndo tutanufaika na kazi ngumu tuifanyayo.
Tumekuwa tukiziweka nyimbo zetu kwenye websites kama Mkito ili walau kila shabiki aweze kuchangia kiasi kidogo katika kazi kubwa tunayoifanya ya kuumiza vichwa na kutunga tungo zenye maudhui ya kuburudisha na kuelimisha jamii.
Lakini wapo watu wachache ambao wamekua wakizi-download nyimbo zetu na kuzi Upload kwenye site zao kama (Blogs, Hulkshare, soundcloud). Kwa kufanya hivyo ni kinyume na taratibu za wasanii wengi, hasa mimi mwenyewe.
Kwasababu vitendo hivyo vinarudisha sana nyuma maendeleo yetu, kwa kiasi kikubwa yanapatikana kutokana na kazi zetu za sanaa.
Hivyo basi, kwa upendo nilionao kwa mashabiki wangu na watu wote kwenye tasnia hii ya muziki, nawaomba nyimbo zangu zisiwekwe kwenye websites nyingine yoyote ile bila ridhaa yangu. Kwani kwa kuweka nyimbo zangu kwenye websites na blogs ambazo sijaziridhia, ni kuninyima haki yangu ya kimsingi ya kupata matunda ya kazi yangu.
Nina upendo mwingi na wa dhati sana na mashabiki wangu, kwasababu mmelilea na kunitunza kisanii tangu siku ya kwanza nilipoachia wimbo wangu wa TAFSIRI, hivyo ningependa upendo huo udumu milele na milele. Maana naamini wengi wenu mngependa kuniona nikiendelea kisanii.
I hope hii haitaleta mitazamo tofauti na nia yangu ya kuwaandikieni ujumbe huu.
Nawapenda Sana…
Blogger Comment
Facebook Comment