AFRIKA KUSINI YALIPA JUKUMU JESHI! KUSHUGHULIKIA WENYEJI WANAOSUMBUA WAHAMIAJI

Jeshi nchini Afrika kusini limeanza kuelekea kwenye maeneo ambayo yameathiriwa na wimbi la machafuko dhidi ya wahamiaji kutoka nchi nyingine za Afrika.

Wanajeshi wanafanya doria katika baadhi ya majimbo ya Kwa-Zulu Natal na Gauteng , pia mjini Alexandra uliopo jiji la Johannesburg ambako Raia wa Msumbiji aliuawa na wengine raia wengine kadhaa kutoka Zimbabwe walinusurika na shambulio.
Watu wameonekana katika makundi wakiwa wamebeba mishumaa karibu na jengo la Mahakama kuu mjinin Johannesburg wakitoa wito wa kukomesha machafuko,ambayo yamegharimu maisha ya watu saba.
Mashambulizi haya yamezusha ghadhabu katika nchi nyingine za kiafrika.
Mnamo mwaka 2008, Jeshi la Afrika kusini lilisambazwa nchini humo baada ya Watu 63 kuuawa kutokana na mashambulizi ya wenyeji dhidi ya wageni
    Blogger Comment
    Facebook Comment