Katika uamuzi wa shauri hilo la madai Namba 13/2011 uliotolewa hivi
karibuni, Mahakama Kuu imeiagiza halmashauri hiyo kumlipa Mwamini
shilingi milioni 20 kutokana na kilema alichopata kwa kuondolewa mfuko
wa uzazi na kukatwa utumbo. Pia, mahakama imeiagiza halmashauri hiyo
kumlipa Jafari fidia ya shilingi milioni tano ikiwa ni gharama za
uendeshaji wa shauri hilo.
Akisoma hukumu, Jaji Mfawidhi wa
Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, Amir Mruma alikubaliana na madai ya
walalamikaji kuwa madhara waliyopata kutokana na uzembe uliofanywa na Dk
Jackob Kamanda ni makubwa.
Jaji Mruma alisema haipingiki kwamba huo ni uzembe uliofanywa na mtumishi, hivyo mwajiri anapaswa kulipa gharama.
Aliagiza
kuwa kiwango hicho cha fedha kitalipiwa riba ya asilimia saba kila siku
kuanzia tarehe ya uamuzi ulipotolewa hadi siku mlalamikiwa atakapolipa
fedha hizo.
Mwamini na mumewe walifikisha malalamiko yao Mahakama
Kuu, wakidai kulipwa fidia ya shilingi milioni 505 kutokana na makosa ya
uzembe uliofanywa na wataalamu wakati wa upasuaji kwa kuacha kitambaa
tumboni mwa mgonjwa.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake,
Anatory Lukonge wa Hospitali ya Itigi ambako walibaini kitambaa tumboni
mwa Mwamini, aliieleza mahakama kuwa walipomfanyia upasuaji walikuta
utumbo umeshikana na kizazi huku juu yake kukiwa na kitambaa.
Dk
Lukonge alisema walikitoa kitambaa hicho lakini kutokana na sehemu ya
kizazi kuharibika, iliwalazimu kukiondoa huku akidai kuwa hali hiyo
ilisababishwa na uzembe wa daktari aliyemfanyia upasuaji.
Blogger Comment
Facebook Comment