Rais Peter Mutharika wa Malawi ametoa salaam za rambirambi kufuatia kifo
cha mwandishi wa habari wa BBC nchini humo Raphael Tenthani, ambaye
amekufa katika ajali ya gari.
Bwana Mutharika amesema, Tenthani atakumbukwa kama mtu mwenye kipaji cha hali ya juu, mcheshi na mchangamfu.
Raphael
Tenthani ambaye alikuwa na umri wa miaka 43 alifahamika nchini kote
Malawi na amekuwa akiripotia Idhaa ya Kiingereza ya BBC kwa zaidi ya
miaka kumi. Pia alifanya kazi na shirika la habari la Marekani la
Associated Press. Mwaka 2010 alishinda tuzo ya Umoja wa Mataifa ya
Vyombo vya Habari kwa kazi yake kuhusu Malengo ya Maendeleo ya Milenia.
Blogger Comment
Facebook Comment