UINGEREZA KUFANYA UCHAGUZI KESHO


Viongozi wa vyama na wagombea wanafanya kampeni zao za mwisho kuwashawishi wapiga kura wawapigie kura kabla ya kufunguliwa uchaguzi mkuu.


Waziri Mkuu David Cameron ataahidi "kuifanya Uingereza kuwa katika njia ya mafanikio", wakati ambapo kiongozi wa chama cha Labour Ed Miliband ataahidi kuwa na "serikali itakayowajali kwanza wafanyakazi".
Kiongozi wa Lib Dem,Nick Clegg ataahidi hali ya utulivu.
Kura ya maoni inaonyesha hakuna chama kitakachoweza kushinda moja kwa moja kwa wingi wa viti.
Naibu mhariri wa BBC James Landale amesema wanasiasa, wapiga kura na vyombo vya habari wanajaribu kufuatilia kwa kina uchaguzi huo, na kuwafanya wengi kufuatilia kile kitakachotokea iwapo matokeo yatakuwa kinyume na matarajio yao.
"Alhamisi, huenda isiwe mwisho wa mchakato huo wa uchaguzi," amesema.
"Huenda uchaguzi huo ukaenda katika hatua ya pili baada ya kushindwa kumpata mshindi wa moja kwa moja."
Katika habari nyingine za uchaguzi mkuu:
■Mgombea wa chama cha UK Independence Party (UKIP) aliondolewa katika kinyang'anyiro cha uchaguzi huo baada ya kupigwa picha akimtishia kumpiga risasi mpinzani wake kutoka chama cha Conservative. ■Kiongozi wa Labour Ed Miliband amesema haamini kama chama chake kitakopa zaidi ya ilivyokuwa mipango ya chama cha Conservative iwapo kitashinda uchaguzi
    Blogger Comment
    Facebook Comment