WALIOOKOKA KWENYE MIKONO YA BOKOHARAMU WAELEZEA MATESO

WANAWAKE NA WATOTO WALIOKUWA WAKISHIKILIWA NA KUNDI LA BOKO HARAM NCHINI NIGERIA WAELEZA BAADHI YAO WALIULIWA KWA KUPIGWA MAWE WAKATI JESHI LILIPOKARIBIA KUWAOKOA


Walikuwa wakizungumza siku moja baada ya karibu mateka mia tatu kuokolewa kutoka msitu wa Sambisa na kuwapeleka katika kambi ya serikali.
Mwanamke mmoja ambaye alijifungua akiwa mateka ameelezea namna wapiganaji hao walivyomkata koo mumewe wake mbele yake, kabla mwanamke huyo kutenganishwa na watoto wake wengine watatu.
Mwandishi wa Associated Press ambaye aliotembelea kambi hiyo amesema wengi wa watoto waliokolewa walikuwa wanaugua utapiamlo mkali.
Jeshi la Nigeria limesema limewaokoa zaidi ya watu mia saba katika kipindi cha wiki moja iliyopita wakati wa mapigano makali yanayoendelea dhidi ya Boko Haram
    Blogger Comment
    Facebook Comment