James Horner, mtunzi nguli wa eneo maarufu kwa watu maarufu la Hollywood
ambaye aliandika na kushinda katika tuzo za Oscar juu ya filamu maarufu
ulimwenguni ya Titanic,amefariki dunia mjini California kutokana na
ajali ya ndege akiwa na umri wa miaka 61.
James alipata mafunzo ya urushaji wa ndege,inaarifiwa alikuwa peke
yake wakati alipopata ajali hiyo,na ndege binafsi ndogo ambayo alipata
nayo ajali eneo la Kusini mwa Santa Barbara mwanzoni mwa wiki hii .
Mwandishi
huyu na mtunzi wa tungo mbali mbali ametia mkono wake katika kazi tatu
tofauti za filamu za msanii James Cameron , pamoja na filamu ya A
Beautiful Mind, Braveheart, Troy na ile ya Apollo 13.katika utendaji
kazi wake uliotukuka, James alipewa tuzo ya Oscar kwa filamu ya Titanic
na wimbo uliotawala humo na nyinginezo .
James alipewa tuzo ya
ushirika katika tuzo ya pili kwenye mashairi na msanii Will Jennings kwa
wimbo bora wa asili , na kwa mafanikio makubwa waliyoyapata katika
wimbo maarufu wa My Heart Will Go On, ambao uliimbwa na Celine Dion.
Ajali
hiyo ilitokea katika msitu mzito wa taifa la Marekani wa Los Padres,
Kaskazini mwa Los Angeles, wakati ndege hiyo ikidondoka ilitoa mshindo
mkuu na kuripuka mara tu ilipotua aridhini moto ambao baadaye ulizimwa
na kikosi cha wazima moto wa eneo hilo. Wanaeleza mashuhuda ambao ni
wazima moto.
Msaidizi wa marehemu Horner , Sylvia Patrycja
amethibitisha juu ya kifo hicho kwa kuandika kweny ukurasa wake wa
facebook mwanzoni mwa wiki hii akisema kuwa: "tumempoteza mtu wa kipekee
sana ambaye alikuwa na moyo mkuu wa kujitoa na mtu mwenye kipaji
kisicho elezeka .amekufa wakati anafanya kitu akipendacho. Asante kwa
mchango wako mkubwa na upendo uliokuwa nao tutaonana mbinguni ."
Blogger Comment
Facebook Comment