Recent

UNAFAHAMU KUWA NYAMA YA MBWA YAWEZA KATISHA MAISHA YA BINADAMU!? NIMEKUWEKEA HAPA

Kuna baadhi ya nchi kama China wana desturi ya kula nyama ya mbwa hata baadhi ya makabila ya hapa Tanzania inadaiwa hutumia nyama ya mbwa kama kitoweo.

Pamoja na ulaji huo ambao wengi wao wanaamini hauna madhara, kuna taarifa kutoka Nigeria zinazohusisha watu watano kupoteza maisha baada ya kudaiwa kula nyama hiyo wakiwa katika hoteli moja ambayo ni maarufu kwa ulaji wa nyama ya mbwa.
Brain Ogbondah ambaye ni mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo alisema watu hao waliripotiwa kufa ikiwa ni muda mchache baada ya kula nyama hiyo iliyoandaliwa na Friday Dickson.
Uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea na viongozi wa familia wamewataka watu kuacha kula nyama hiyo.


Habary hii imeandikwa na Dj Alchama ikitoka kwenye ukurasa wa Millardayo.com

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment