Hizi ndio sababu za Facebook kuamua kufungua office zao Africa..
Nimeipata hii takwimu ambayo sikuwa nafahamu, kumbe Facebook ina watumiaji Milioni 120 wa Mtandao huo ndani ya Africa pekeyake !!
Story nyingine kuhusu Facebook
kwa sasa hivi ni ishu ya kusogeza Office zao mpaka ndani ya Jiji la
Johannesburg Afrika Kusini na tayari hapo ndio yatakuwa Makao Makuu ya
shughuli zao zote zinazohusu Facebook Afrika, Nunu Ntshingila ndio Boss ambaye kachukua ajira kusimamia Kampuni hiyo.
Facebook iliangalia siku nyingi
sana jinsi ya kuingia kwenye soko la Afrika, waliwahi kurahisisha huduma
kwa watumiaji wa mtandao huo kwa kuweka App maalum ambayo mtumiaji
hakatwi pesa wala hatumii data kwenye kuchat, mpango wao mwingine ni
kuhakikisha wanamfikia kila mtu hata ambae hana uwezo wa kumiliki simu
yenye uwezo wa Internet.
Blogger Comment
Facebook Comment