Recent

JOSE MORINHO AFUKUZWA CHELSEA!

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya England, Chelsea wameendelea kuwa na bahati mbaya baada ya kuendelea kupata matokea mabaya mfululizo.
Kilichonifikia leo ni kuhusu kocha wa klabu hiyo Jose Mourinho kufutwa kazi baada ya kuendelea na matokeo mabaya mfululizo…uamuazi huo unaufanya uongozi wa klabu hiyo kumlipa kiasi cha pauni milioni 40 kama sehemu ya mkataba wake.

Bodi ya klabu hiyo chini ya mmiliki wa klabu hiyo, Roman Abramovich ilikuwa na kikao kizito jana kujadili hatma ya Mourinho na kufikia uamuzi huo.
Mourinho mwenye umri wa miaka 52 amekuwa na Chelsea kwa kipindi cha pili mfululizo na msimu uliopita walifanikiwa kutwaa ubingwa huku msimu huu mpaka sasa wakiwa tayari wamepoteza michezo tisa kati ya 16.
Mara ya mwisho Chelsea imepokea kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Leicester Cityna kuwakatisha tamaa kabisa mashabiki wake.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment