{AUDIO} DIAMOND PLATNUMZ AYAKATALIA MAKAMPUNI KAMA SONY KUFANYA NAE KAZI! AELEZA SABABU ZAKE HAPA!

Msanii wa muziki wa bongo fleva anaepaparusha vyema bendera ya nchi yake kimataifa Diamond Platnumz amefunguka kwamba ameshayakatalia makampuni mengi na makubwa sana duniani kufanya nae kazi kwa sababu anadai haoni faida yake!
Mkali huyo kutoka Bongo Tanzania anaetamba na Hit kibao zilizo fanya vizuri Afrika na Duniani kote kama Make me sing, Nana aliyofanya na mkali Mr Flavour kutoka Nigeria na nyingine kibaao amedai kwamba- Ili msanii usaini kufanya kazi na kampuni fulani ni lazima uwe umekwama au unahitaji msaada kwa nyanja fulani!
akaendelea kudai kwamba yeye uwezo wa ku record na kufanya videos anao kuanzia yeye mpaka kwa wasanii wake! kwahiyo haoni sababu ya yeye kufanya kazi na makampuni hayo kwa sababu hayato msaidia lolote.
Sikiliza hapa alipohojiwa na Perfect Crispin wa Clouds FM
    Blogger Comment
    Facebook Comment