Tim Cook amesema baada ya kimya cha muda
mrefu ambacho amekuwa akitunzia siri hiyo, ameona namna alivyonufaika
kutokana na kitendo cha watu wengine kujitoa sadaka kwa kijitangaza na
kusisitiza kuwa anajivunia kuwa shoga na anajiona mwenye zawadi kubwa
kutoka kwa Mungu.
Amesema kitendo cha yeye kama mkurugenzi
wa kampuni hiyo kujitangaza kitawafanya wengine wenye hali kama yake
wajione wako sawa na watu wengine.
Cook amesema marafiki zake wanajua kuhusu suala la yeye kuwa shoga, na haifanyi wamchukulie tofauti na watu wengine.
Kabla ya kujitangaza kumekuwa na fununu
kuhusiana na Cook kuwa shoga, anakuwa mkurugenzi wa kwanza wa kampuni
kubwa kujitangaza kuwa shoga ambapo mwaka jana alikuwa moja ya watu
waliokuwa wanaunga mkono sheria ya kuwalinda wafanyakazi
wasinyanyapaliwe kutokana na jinsia zao.
Cook amesema kwa kipindi kirefu watu wamekuwa wakificha juu ya jambo hilo maeneo ya kazi kuepuka unyanyapaa.
Blogger Comment
Facebook Comment