Viongozi wa ligi kuu ya Uingereza klabu ya Chelsea leo ilisafiri mpaka
jijini Liverpool kwenda kucheza na vijana wa Roberto Martinez –
Everton.
Mchezo huo uliopigwa katika dimba la Goodson Park umemalizika kwa
Chelsea kuendelea kuimarisha uongozi wao wa pointi 7 baada ya kuifunga
Everton 1-0.
Goli pekee la Willian katika dakika ya 89 lilihakikishia Chelsea ushindi muhimu dhidi ya Everton.
Wakati huo huo Manchester City imeifunga Stoke City 4-1. Magoli
mawili ya Sergio Aguero na moja Milner na lingine la Samir Nasri
likahatimisha ushindi huo wa City ambao wamekuwa na mfululizo wa matokeo
mabaya siku za hivi karibuni.
Blogger Comment
Facebook Comment