Shule zote nchini Niger zinafungwa kwa siku kadha wakati nchi hiyo
inapojaribu kukabilian na mlipuko wa ugonjwa wa uti wa mgongo au
meningitis, ambao umewaua zaidi ya watu 80 mwaka huu
Waziri mkuu Brigi Rafini amezindua shughuli ya kutoa chanjo kwa
watoto wote kati ya miaka mwili na kumi na tano, lakini akasema kuwa
Niger ina nusu tu ya madawa yanayohitajika ambapo alitoa wito kwa
shirika la afya duniani WHO kwa msaada zaidi.
Waziri wa afya
nchini humo amewaonya watu akiwataka kuacha kutumia madawa
yasiyoidhinishwa akisema kuwa dawa hizo zinaweza kuwa za aina tofauti ya
ugonjwa huo.
Asilimia kubwa ya visa 900 vya ugonjwa huo vilivyoripotiwa vimekuwa mji mkuu Niamey na magharibi mwa nch
Home / Uncategories / UGONJWA WA UTI WA MGONGO WALETA MAAFA NCHINI NIGER! WASABABISHA SHULE ZOTE KUFUNGWA!
Blogger Comment
Facebook Comment