Mazungumzo juu ya mpango wa nuklia wa Iran yanarejelewa tena mjini
Vienna wakati wapatanishi wanapojaribu kupata makubaliano ya mwisho
yaliyoafikiwa wiki tatu zilizopita.
Makubaliano hayo yalitajwa kuwa ya kihistoria. Sasa maafisa kutoka
mataifa sita yenye nguvu duniani na Iran yanakabiliwa na wakati mgumu wa
kujaribu kuchambua masuala ya kina kabla ya mwisho wa mwezi juni.
Iran itahitajika kuacha kurupisha madini ya Uranium ili nayo iwezi kuondolewa vikwazo ambavyo vimeuporomosha uchumi wake.
Maafisa
nchini Marekani wanase kuwa waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani
Johh Kerry huenda akakutana na mwenzake wa Iran Mohammad Javad Zarif
mjini New York siku ya Jumatatu
Blogger Comment
Facebook Comment