Nchi ya saudi arabia yatangaza rasmi kumaliza kampeni zake za mashambulizi zidi ya waasi wa kutoka yemen
Lakini wamesema Vikosi vya kijeshi vitatumika tu ikiwa vitahitajika, na operesheni zinaweza kuendelea kwa kiasi.
Iran ambayo inawaunga mkono waasi, imeelezea kauli ya Saudi Arabia kuwa ya kupiga hatua.
Nae Msemaji wa ikulu ya Marekani, Josh Earnest,amesema Marekani imezitaka pande zote mbili zilizo kwenye mgogoro nchini Yemen, kufanya mazungumzo ili kupata suluhu.
Baada ya kampeni za mashambulizi ya mwezi mmoja zilizotekelezwa na Sudi Arabia, Serikali ya Yemen bado haijarejeshwa.Kadhalika wanamgambo wa kihuthi bado wanadhibiti mjini mkuu, Sanaa.
Blogger Comment
Facebook Comment