Naibu waziri wa ulinzi nchini Ugiriki amezitaka nchi za kaskazini mwa
bara Ulaya kufanya juhudi zaidi kuwaokoa wahamiaji kutoka bahari ya
Mediterranean.
Kostas Isichos aliiambia BBC kuwa kile Ulaya ingefanya ni kugawana majukumu ya kukabiliana na janga hilo la kibinadamu.
Amesema
kuwa walinzi wa pwani wa Ugiriki wamelemewa na idadi ya wahamiaji na
wanahitaji mashua zaidi na helkopta ili kuweza kuokoa maisha.
Pia
bwana Isichos amezitaka nchi zingine kuwakubali wahamiaji zaidi. Jeshi
la wanamaji la Uingereza linaripotiwa kutathmini msaada ambao litatoa.
Wahamiaji
zaidi waliondolewa baharini jana Jumanne na viongozi wa bara Ulaya
watazungumzia suala hilo kwenye mkutano ambao utaandaliwa mjini Brussels
hii leo
Blogger Comment
Facebook Comment