NkurunzizaRais Jakaya Kikwete wa Tanzania ambaye kwa sasa ni mwenyekiti
wa Jumuia ya Afrika Mashariki amewataka mawaziri wa mambo ya nje kutoka
nchi wanachama kufanya mazungumzo nchini Burundi, Jumatano kabla ya
mkutano wa viongozi wa jumuia hiyo.
Mindi Kasiga mkuu wa kitengo cha mawasiliano kwa umma katika wizara
ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa nchini Tanzania na kusema
mazungumzo hayo yanatarajiwa kuwa ya kwanza kufanyika kuelekea kikao cha
dharura cha wakuu wa nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki.
Hii ni
mara ya kwanza kwa jumuia hiyo kutuma ujumbe wa ngazi ya mawaziri kwenda
Bujumbura katika jitihada za kujaribu kumaliza mgogoro wa kisiasa
katika nchi hiyo ambayo kwa miaka mingi imekuwa katika vita vya wenyewe
kwa wenyewe.
Hatua hiyo imekuja wakati ambapo viongozi wamekosolewa kwa kukaa kimya huku hali nchini Burundi ikizidi kuzorota.
Waziri
wa mambo ya nje wa Burundi Laurent Kavakure alikuwa nchini Tanzania
jana Jumatatu ambako alifanya mazungumzo na waziri mwenzake wa mambo ya
nje wa Tanzania Bernard Membe kabla ya kutolewa kwa taarifa hiyo.
Chama
cha Msalaba Mwekundu nchini Burundi kimesema watu wapatao kumi na
wawili wameuawa tangu maandamano kuanza tarehe 26 Aprili baada ya Rais
Pierre Nkurunziza kuteuliwa na chama chake tawala cha CNDD-FDD kugombea
katika uchaguzi wa Juni mwaka huu.
Blogger Comment
Facebook Comment