POLISI NCHINI ISRAEL WAKIWA JUU YA FARASI WAMEKABILIANANA WAANADANAJI KUTOKA MAKUNDI YA WAYAHUDIWENYE ASILI YA ETHIOPIA AMBAO WANADAI KUBAGULIWANA POLISI WA TAIFA HILO
Katika maandamano hayo yalitokea Tel Aviv, Polisi walitumia mabomu ya
machozi na maguruneti kuwatawanya mamia ya waandamanaji hao. Watu kadhaa
wamejeruhiwa wakiwemo maafisa wa Polisi 20. Wayahudi wenye asili ya
Ethiopia waliitisha maandamano kufuatia picha za video zilizosamabaa
wiki iliyopita ambazo zinaonyesha askari wenye sare wenye asili ya
Ethioppia wakiteswa na Polisi. Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
ametoa wito kurejesha hali ya Amani na kuahidi kuwa polisi watafuatilia
tuhuma hizo na kuzifanyia uchunguzi wa kina
Blogger Comment
Facebook Comment