WANAWAKE NA WATOTO WALIOKUWA WAKISHIKILIWA NA KUNDI LA BOKO HARAM NCHINI NIGERIA WAELEZA BAADHI YAO WALIULIWA KWA KUPIGWA MAWE WAKATI JESHI LILIPOKARIBIA KUWAOKOA
Walikuwa wakizungumza siku moja baada ya karibu mateka mia tatu
kuokolewa kutoka msitu wa Sambisa na kuwapeleka katika kambi ya
serikali.
Mwanamke mmoja ambaye alijifungua akiwa mateka ameelezea
namna wapiganaji hao walivyomkata koo mumewe wake mbele yake, kabla
mwanamke huyo kutenganishwa na watoto wake wengine watatu.
Mwandishi
wa Associated Press ambaye aliotembelea kambi hiyo amesema wengi wa
watoto waliokolewa walikuwa wanaugua utapiamlo mkali.
Jeshi la
Nigeria limesema limewaokoa zaidi ya watu mia saba katika kipindi cha
wiki moja iliyopita wakati wa mapigano makali yanayoendelea dhidi ya
Boko Haram
Blogger Comment
Facebook Comment