Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, amepuuzia wito uliotolewa na nchi ya
Marekani pamoja na umoja wa Ulaya juu ya wito uliotolewa kuhusu uchaguzi
uahirishwe
Rais Nkurunziza ameiambia BBC kwamba kuahirishwa kwa uchaguzi
kutaliingiza taifa hilo katika mgogoro mkubwa zaidi."unapoona asilimia
tisini na tisa ya nchi yote ina amani na usalama hii ina maana mazingira
yanaruhusu uchaguzi kufanyika .
Unaweza kusema kwamba uchaguzi
usitishwe ikiwa watu wote wanazungumza lugha hiyo ya kusitishwa kwa
uchaguzi ,na hiyo itakuwa na maana kwamba tutakuwa na serikali ya mpito.
Hatuwezi
kukubaliana na wito huo hata kidogo hapa nchini Burundi,kwasababu
kukubaliana na wito huo ni kukaribisha vurugu kubwa zaidi na matatizo
makubwa zaidi mbeleni hasa tukiunda serikali ya mpito."
mpaka
sasa watu tisa wamepoteza maisha yao katika vurugu zilizo dumu kwa wiki
ya pili sasa ,vurugu zenye lengo la kukinza maamuzi ya rais wa nchi
hiyo Nkurunziza asigombee nafasi ya urais kwa muhula wa tatu.
Kufuatia
vifo hivyo rais Nkurunziza amesema kwamba anasikitika kutokana na vifo
hivyo,na kwamba vurugu hizo zimesababishwa na kile anacho kielezea kama
ushawishi kutoka mataifa mengine:
"kwa kawaida unapozungumzia juu
ya suala la maandamano sio suala la kwenda kuua watu wala kuwashambulia
polisi na hata kuchoma moto magari na kadhalika.
Ina maana kwamba
yakitukia mabo kama hayo wakati wa maandamano basi hayo siyo
maandamano,hiyo ni sawa na vita,ndiyo maana tunasikitika kutokana na
vifo vilivyotokea wakati wa maandamano hayo lakini ni lazima tuwe na
maamuzi ya kusitisha vurugu na hivyo basi kuwaruhusu watu kuingia kwenye
harakati za uchaguzi."
Blogger Comment
Facebook Comment