Mkuu wa sera za mambo ya nchi wa Umoja wa Ulaya, Federica Mogherini
ametahadharisha kwamba tatizo la uhamiaji katika bahari ya Mediterranea
ni kubwa na linahitaji utatuzi wa kipekee.
Akilihutubia baraza la usalama la umoja wa mataifa, Federica
Mogherini amesema kipaumbele kwa bara la Ulaya sharti iwe ni kuokoa
maisha katika eneo la bahari- lakini amesisitiza kwamba hakuna miujiza
katika kupata utatuzi wa hilo. Amesema hakuna mhamiaji au mkimbizi
atakae rudishwa bila ridhaa yake.
"lazima tukubaliane na ukweli
kwamba kuna makundi ya kihalifu, mitandao ya kihalifu inayofanya kazi
mipakani ikiwa na mtandao mzuri kabisa huku wakitengeza fedha nyingi
ambazo zinatumika kuwafanya watu watumwa kutokana na matatizo yao.
Wanawauzia watu matumaini lakini badala ya matumaini wanauawa watu.
Lazima tukabiliane na hilo bila hivyo, itakuwa hatuishi kwa misingi ya
utu wetu na hadhi yetu. Bila shaka, hii haina maana kwamba hatutaweza
kukabiliana na tatizo la kuwatunza watu tuliowaokoa.")
Mapendekezo
mapya ya kukabiliana na tatizo la uhamiaji yatawasilishwa siku ya
Jumatano wiki hii na Tume ya Umoja wa Ulaya. Mapendekezo hayo
yatajumuisha mipango ya kuwepo kiwango maalumu cha wahamiaji ambao
watachukuliwa na nchi zote wanachama wa Umoja wa Ulaya.
Sera ya
Uhamiaji ya tume hiyo itakayotangazwa katikati mwa juma pia itapendekeza
kuwepo kwa hatua za kisheria zitakazowaruhusu wahamiaji kuingia barani
ulaya ili waepukane na kwenda kwa wafanya biashara hara mu ya
kusafirisha watu.
Blogger Comment
Facebook Comment