Wakati kukiripotiwa mvua kubwa na tetemeko kubwa na jipya nchini Nepal,
Wakuu nchini humo wamethibitisha kuwa idadi ya watu waliokufa kutokana
na tetemeko hilo jipya , imepanda na kufikia zaidi ya watu 60.
Wakati huo huo helikopta ya kikosi cha majini cha Marekani,ambayo
ilikuwa ikifanya kazi ya kusaidia kusambaza huduma za kibinaadamu nchini
Nepal, haijulikani.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa, ndani ya
helkopta hiyo kulikuwa na watu nane,miongoni mwao, sita ni askari wa
kikosi cha majini cha Marekani na askari wawili wenyeji wa jeshi la
Nepal.
Maofisa wa serikali wa Marekani wamesema kwamba helkopta
hiyo ilikuwa maeneo ya jirani na kijiji cha Charikot, ambacho
kiliharibiwa vibaya na tetemeko la ardhi.
Blogger Comment
Facebook Comment