HARMONIZE KUFANYA SHOW YA NYUMBANI LEO KWA MARA YA KWANZA!

Msanii Harmonize kutoka WCB lebel inayosimamiwa na msanii Diamond Platnumz! Leo tarehe 27 May atakuwa ana perform kwa mara ya kwanza nyumbani kwao (Mkoani kwao) Mtwara toka alipoondoka huko na kwenda Dar es Salaam kuanza rasmi safari yake ya kimuziki.


Msanii huyo amakuwa na mafanikio kimuziki baada ya kutengeneza HIT kadhaa kama Aiyola na Bodo ambayo amemshirikisha Bosi wake Diamond Platnumz.
Show hiyo ambayo anaifanya leo huko Mtwara inaitwa BADO KIBOKO KABISA iliyoandaliwa na mwanadada NIsha kutoka Bongo Movie.
tukiachana na Harmonize show hiyo pia ita pambwa na wasanii wengine kama Leyla, Mau mchekeshaji kutoka Bongo Movie, Nisha muigizaji wa Bongo Movie pamoja na Crew ya WCB ambayo itaenda kumpa support Harmonize.
Show hiyo itafanyika pale MAKONDE POLICE MESSI
Msanii Harmonize hajawahi kufanya show yeyote katika mkoa wake huo na leo ndo itakuwa mara ya kwanza kwa wana Mtwara kumshuhudia kijana wao huyo katika jukwaa.
Katika picha ni Harmonize katika pozi!
    Blogger Comment
    Facebook Comment