SHILOLE & VANESSA NI KICK AU MTONYO!?

Tarehe 18 ya mwezi huu wa 5 mwaka huu wa 2016 macho ya mashabiki wa muziki wa wasanii hawa wawili yalikuwa katika mitandao ya kijamii hususan ule wa Istagram ambao wawili hawa (Shilole & Vanessa Mdee) walikuwa wakirushiana maneno makali kwa kilicho semekana kwamba walikuwa wametofautiana(Wamegombana).
Ugomvi huo inasemekana kwamba ulianza baada ya Shilole kusikia kwamba Vanessa alimzungumzia vibaya  katika moja ya saloon ambazo wawili hao hupenda kutembelea!
Wawili hao walichukua headlines kwa wakati huo kwa kila mmoja kumtupia mwenzie maneno kadri alivyo weza huku kila mmoja akijitapa katika ukurasa wake wa mtandao huo wa Instagram!
Ni siku 9 tu toka tukio hilo lipite hadi sasa!
Jumapili hii ya tarehe 29  pale Club BILZ kuna show imeandaliwa ya wawili hao kufanya Show katika jukwaa moja! mpaka sasa haijafahamika kwamba wawili hao walitumia ile kama KICK ili kuitengenezea mazingira show hii ambayo wamaiandaa, au kuna mtu ametokea kuidhamini hiyo na akawapa mtonyo (Pesa) ili kulikamilisha hilo!?
Bado haija fahamika lakini ukweli upo ndani ya mioyo yao! kamani kick walitumia ili kuiandalia mazingira show yao au ni pesa ndo zimewasogeza kufanya show ya pamoja.



    Blogger Comment
    Facebook Comment