Msanii Rich Mavoko ambaye yuko chini ya record label ya WCB Wasafi amefunguka yamoyoni jana June 2 baada ya kusaini mkataba rasmi na kuwa mwanachama wa record label hiyo.
Alizungumza hayo wakati alipokuwa akihojiwa nnna BDOZEN wa Clouds FM katika kipindi cha XXL walipotembelea redioni hapo kwa ajili ya kutambulisha nyimbo yake mpya ambayo ameifanya chini ya record label hiyo.
Hiyo ni baada ya kukutanishwa na waandishi wa habari asubuhi hiyo ya jana na kuweza kudondosha wino mbele ya vyombo vya habari.
+Rich Mavoko amesema yupo katika mikono salama kwa sababu ana imani na management aliyonayo kwamba itamfikisha mbali na kuweza kufanya kazi ambazo mwanzo alikuwa akikwama lakini sasa watafanya kazi kama team.
Msikilize hapa +Rich Mavoko akifunguka.
Blogger Comment
Facebook Comment